World's Last Chance
A New World Order  
  Bible Prophecies
 
ARTICLES
RESOURCES
FOR YOU
SHORT STUDIES
SUBSCRIBE TO OUR UPDATES
Nature Power
Back  
A New World Order Send to a Friend Image of The Beast Print
Read it in the following languages 
FONT SIZE
If you are unable to read this file, then Click Here to download fonts.
 
 
We highly recommend that you also read the Next & Last Pope article after this article
Nafasi Ya Mwisho Ya Dunia Mpangilio Mpya wa Dunia upo Karibu Kuanza: Je! Uko Tayari kwa ajali yake?
 


  • Merekani na papa wanaitaka
  • Kutokea kwake kutakamata ulimwengu
  • Ilitabiriwa miaka elfu mbili iliyopita
  • Vile unavyoweza kuepuka kuwa mhasiriwa wake
  • “Papa Yohana Paulo wa Pili alipiga simu Alhamisi ya Mwaka Mpya na mwito mpya wa … umbaji wa mpangilio mpya wa dunia.” Jan. 2, 2004, Tangazo la Kikristo

    “Ni wazo kubwa: mpangilio mpya wa dunia ... ni Amerika tu ambayo ina uadilifu kamili na umaanisha kuiunga mkono.” Rais wa hapo awali George Bush, hotuba ya Umoja wa Jimbo, Jan. 29, 1991
    In this article:

    Ulimwengu wetu hivi karibuni (kwa miaka badala ya karne) utakabiliana na shida duniani kote ambayo itatangaza mwisho wake. Kwasababu watu duniani kote wanahitajika kujitayarisha, tunapeleka ujumbe huu kwa mataifa mengi, kwa gharama kuu na kwa kujitolea.

    Kwa wale ambao watakao thubutu kuendelea kusoma, Nafasi Ya Mwisho ya Dunia inaweza kuwa upuzi, kama si ovyo, kwasababu kwa kawaida unatumaini amani duniani na fanaka, na kwa hakika si shida itakayo kabili ulimwengu na kuimaliza.

    Tumejaribu kuona majibu yako na maswali na tutaanza safari hii ya maisha ya usoni kwa kujibu baadhi ya maswali yako tunaposhirikiana nawe ni kwanini ulimwengu huu unaangalia nafasi yake ya mwisho!

    Biblia kama Mwongozo

    1. Je! Ni akina nani waliyo nyuma ya nakala hii?

    Sisi ni sehemu ya kikundi kidogo cha watu waliyotawanyika ulimwenguni kote ambao wanachukulia Biblia kuwa amri yetu tu. Baada ya kutoa muda kadhaa kuisoma, sana sana milango inayoelekezea maisha yetu ya usoni, tumegundua ni lazima tushiriki na wewe kile ambacho tumejifunza. Ufahamu huu ni wa maana sana hadi tukotayari kuvumilia ugumu na kujitolea, hata maisha yenyewe, ili iweze kupatikana kwako. Ngome zenye nguvu zinafanya kazi sana kunyamazisha maelezo haya.

    2. Je! Ni kwanini unachukulia Biblia kwa umakini sana?

    Hapo awali hatuchukulia Biblia kwa umakini sana hadi tuliposhangaa kugundua vile ilivyo sahihi. Sahihi sana, hadi utabiri uliyofanywa miaka elfu iliyopita ilifanyika siku ile iliyotabiriwa kwa ukamilifu. Hii ilitufanya tukamilishe kuwa kuna Mungu anayejua yote nyuma ya Biblia, ambaye hafungwi na muda na anajua mwisho kutoka kwa mwanzo.

    Tulijifunza pia kuwa Muumbaji wetu anatupenda sisi sana hadi alitayarisha pahali kwa ajili yetu mbinguni. Walakini, kwa kuwa tumeambukizwa na ugonjwa wa dhambi na kwa sasa hatufai kuishi na Mungu mbinguni, Mungu alitayarisha dawa ya ugonjwa wa dhambi.

    Hatungechukulia Biblia kwa umakini sana kama Mungu hangeonyesha utawala kamili kama huo na ufahamu wa maisha ya usoni. Utawala huu unafafanuliwa wazi sana katika vitabu viwili: Danieli katika Agano la Kale na Ufunuo katika Agano Jipya.

    Tabiri za Biblia zilizo Timilika.

    3. Peana mfano wa utabiri uliyokamilika kwenye Biblia.

    Katika kitabu cha Danieli, mlango wa pili, Mungu alionyesha katika ndoto mfalme wa Babeli kuwa kwanzia wakati wake hadi wakati wa mwisho, ulimwengu utashuhudia falme nne duniani peke yake. Historia imedhibitisha kuwa cho chote ambacho Mungu alikiteua mbeleni ni kile ambacho kwa kweli kilifanyika. Falme nne zilikuwa, Babeli (605 BC-538 BC), Uajemi (538 BC-331 BC), Uigiriki (331 BC- 168 BC), na Roma (168 BC-476 AD). Alifafanua zaidi kuwa Roma itagawanyishwa katika majimbo kumi na kuwa katika wakati wa majimbo haya mwisho wao utakuja. Historia imehakikisha usahihi wa neno la Mungu. Kwa kuwa kuwadia 476 AD, Roma iligawanyishwa katika mataifa kumi ambayo Uropa ya sasa ilitokea.

    Kwa kuongezea, Mungu alionyesha maelezo ya kipekee ya kila ufalme, kama vile hali ya vile watakavyo inuka kuwa na nguvu na kuanguka, na tabia za maana za kila serikali. Angalia Danieli 7 na 8. Maelezo ya kutosha yalipeanwa ambayo mwanafunzi aliye na fikira wazi wa historia na Biblia hawezi mbali kukubali kuna Mungu mbinguni ambaye anatawala ulimwengu wetu.

    4. Je! kusudi la tabiri za Biblia ni nini ?

    Kusudi la unabii ni kutuonya sisi kuhusu shida za maisha ya usoni. Kwa mfano, Mungu alimuonya Nuhu kuhusu gharika iliyokuwa inakuja, Abrahamu na Lutu kuhusu kuangamizwa kwa miji ya Sodoma na Gomora na Akamwambia Musa kuhusu tauni za Misri. Iliwabidi wote watii onyo kwa imani. Matukio haya yalinakiliwa ili kutufunza sisi kuwa cho chote ambacho Mungu alikitabiri kilifanyika vikamilifu kama alivyosema. Hivyo basi, hatuwezi kupuuza unabii wo wote Wake ambao haujakamilika kwa kuwa yanatumika kama onyo ya kuwa, tukitii, itatulinda kutokana na shida.

    Kwa hivyo, unabii wa Biblia unamatumizi mawili - kupendeza akili zetu kuhusu kuwepo kwa Mungu ambaye yupo kwenye husukani wa matukio yote na, kutuonya sisi kuhusu hali ya mauti.

    Onyo la kutisha sana na la Kutuliza Moyo

    5. Je! Kuna onyo la kinabii katika Biblia ambalo halijakamilika bado?

    Kwa kweli, onyo la kinabii la kutuliza moyo sana bado halijakamilika. Sasa, hakuna cho chote cha muhimu sana kwetu kuelewa kama unabii huu kwasababu matukio yanafanyika kwa haraka ili kuonyesha kukaribia kukamilika kwake.

    6. Shiriki nami onyo la kinabii la kutuliza moyo sana ambayo ikokaribu kukamilika.

    “Na mwingine, malaika wa tatu,akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo myama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo: Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele: wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake. Hapa ndipo penye subira ya watakatifu: hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu” Ufunuo 14: 9-12.

    Onyo hili la kutisha ufafanua vikundi viwili vya watu. Kikundi cha kwanza kimeonywa dhidi ya kuabudu mnyama na sanamu yake, ambayo huwaongoza kupokea chapa ya myama; wakati kikundi cha pili uonekana kutunza sheria za Mungu vyema. Cha ziada, ufafanuzi wa kurudi kwa pili kwa Kristo ufuata kwa usambamba onyo hili. Kwa hivyo, tunajua kuwa hili ndilo onyo la mwisho lililopeanwa kabla ya kurudi kwa pili kwa Kristo.

    7. Ninawezaje kukwepa kumuabudu mnyama na sanamu yake na kupokea chapa yake?

    Swali nzuri. Ndiposa kuijibu inatupasa kutambua mnyama, sanamu ya mnyama, na chapa ya mnyama. Ni kawaida kudhania kuwa Mungu hawezi kutuonya kuhusu vitu hizo za hatari bila kutusaidia sisi kuzitambua katika njia ya kutamatisha. Mungu wetu mwenye upendo hawezi kutufanya sisi tudhanie, wakati umilele wa milele hupo hatarini. Bila kushangaza basi, tunapata ufafanuzi wa mnyama na sanamu yake katika milango iliyotangulia ambapo vifunguo vingi vinapeanwa ili kufungua utambulisho wao.

    Kumtambua Mnyama

    8. Je! Biblia inamfafanua aje mnyama huyu?

    “Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. 2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba: yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. 3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti; na pigo lake la mauti likapona: Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. 4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake: nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? 5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. 6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. 7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda: akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. 8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu,kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia... 16 Naye uwafanya wote,wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: 17 Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapo ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huo: maana ni hesabu ya kibinadamu; na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita” Ufunuo 13: 1-8, 16-18.

    9. Kifungu kilicho hapo juu kimejaa ishara. Nawezaje kuielewa?

    Tunapaswa kuacha Biblia itafsiri ishara zake yenyewe. Tunapaswa kutarajia kuwa Mungu, kwa faida yetu, alifafanua kwenye Biblia umaana wa ishara hizi. Kwa hivyo, kile tunacho kihitaji ni bidii katika kusoma ili tupate utafsiri kwenye Biblia. Kwa njia hiyo, tunazuiya kudhania na kukisia kwa mwanadamu.

    Kwa kweli Biblia inahukumu kudhania na kukisia kwa mwanadamu kwasababu “hakuna unabii…upata kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu”2 Peter 1:20. Biblia hufafanua ishara zake yenyewe. Kwa mfano, kitabu cha Ufunuo kina mistari 404. Kati ya hizi mistari 404, 278 zinapatikana karibu neno kwa neno katika vitabu vingine kwenye Biblia, ambapo umaana wao umefafanuliwa zaidi.

    Kwa hivyo, tunakuhimiza ufanye kama vile Maberoya wa Biblia (angalia Matendo 17:10,11) na kuleta kila funzo kwa mtihani wa Andiko. Kwa kuwa, ye yote ambaye atasoma Biblia kwa kuomba, akitamani kujua ukweli, ili aweze kuitii, ataelewa Maandiko. “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua ... kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.” Yohana 7:17.

    10. Je! Ni ishara ipi ambayo tunapaswa kuifungua ili kumtambua mnyama na chapa yake?

    Kuna ishara nyingi za mnyama: haitoshi, tutajitosheleza na zile zinazohitajikana ili kumtambua mnyama. Ishara hizi ni ‘mnyama’, ‘joka’, ‘bahari’, ‘miezi arobaini na miwili’, na ‘makufuru’.

    Mnyama: Katika unabii wa Biblia, mnyama ni ishara ya mfalme au ufalme. Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne…huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne…”Danieli 7:17, 23. Na mnyama huyu, tunasoma ufalme wa kitofauti kwa kuwa si nguvu ya kisiasa lakini ya kidini pia, kwasababu watu ‘walimuabudu mnyama’Ufunuo 13:4.

    Joka: Kulingana na Biblia, joka ni jina lingine la Shetani, baba wa utapeli na udanganyifu, “yule joka...aitwaye Ibilisi, na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote.” Hii inaweza kumaanisha kuwa, wakati Shetani alipeana “nguvu zake, na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi” kwa mnyama, tunaweza kutarajia mnyama kufanya njia hizo sawa za udanganyifu za Shetani. Kwa hivyo, hali kubwa ya udanganyifu itapatikana katika shughuli za mnyama. Ufunuo 12:9; 13:2

    Bahari: Katika unabii wa Biblia, bahari ni ishara ya makutano wa watu wengi tofauti tofauti. “… maji …ni jamaa, na makutano, na mataifa, na lugha Ufunuo 17:15. Ikifuatana, ufalme huu wa kipekee au nguvu ziliinuka kutoka baharini, ikimaanisha kuwa ilitoka kutoka kwa eneo ulimwenguni ambalo halikuwa na watu wengi na watu kutoka mataifa tofauti tofauti.

    Miezi arobaini na miwili: Muda huu ni sawa na miaka mitatu na nusu (42 ikigawanywa na miezi 12). Na Biblia iliandikwa msingi wake ukiwa kwa kalenda ya Kiyahudi ambapo kila mwaka wa Kiyahudi ni siku 360 (siku 30 kwa kila mwezi). Kwa hivyo, miaka mitatu na nusu na miezi arobaini na miwili ni sawa na siku 1260. Sababu yetu ya kubadilisha miezi hizi kwa siku zake sawa ni kuwa wakati Mungu aliipa muda unabii, mara kwa mara alibadilisha siku kuwa mwaka “… siku arobaini, kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu,ndiyo miaka arobaini…” “siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia” Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6.

    Kwahivyo, miezi arobaini na miwili ya kiunabii inamaanisha muda wa miaka 1260 ambapo mnyama alipewa, “kinywa cha kunea maneno makuu, ya makufuru” na “kufanya vita na watakatifu na kuwashinda: na akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa” Ufunuo 13:5, 7. Kumaanisha kuwa kupitia wakati huu mnyama atawatukana, kuwatesa Wakristo, na kuwa na uwezo mwingi.

    Kufukuru: Kwenye Biblia, kufukuru imefafanuliwa kwa njia mbili. Ya kwanza ni wakati mtu anasema kuwa yeye ni Mungu au anamwakilisha. “…kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufukuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu Yohana 10:33. Kwa hivyo mnyama, nguvu hii ya dini na siasa na ufalme, imemfukuru Mungu kwa kujifanya kuwa kwenye sehemu ya Mungu ulimwenguni. Njia ya pili ya kufukuru ni kwa kupeana msamaha (kudai kuwa na nguvu za kusamehe dhambi za wengine). “Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?” Mark 2:7.

    Mnyama, nguvu hii ya dini na siasa na ufalme, imemfukuru Mungu si kwa kuchukua nafasi Yake ulimwengu tu, mbali kwa kudai haki ya kusamehe pia. Ndiyo maana mnyama ana “jina la kufukuru” na uzungumza “matusi kinyume na Mungu, na kulitukana jina lake”; hii ni kwasababu mnyama udai nguvu ambazo ni haki kamili ya Mungu peke yake. Ufunuo 13:1, 6.

    Alama Tisa za Maana

    Baada ya kuruhusu Biblia kufungua umaana wa ishara zake, tunaweza sasa kuangazia alama tisa muhimu sana zinazo tambua mnyama ili kuamua ni nguvu ipi katika historia inayotimiza yale yaliyomo. Hizi si vitambulisho peke yake: kuna zingine zaidi kwenye Biblia. Tunatumaini mkusanyiko huu wa vifunguo vya utambulisho vitakuongoza kutafuta kwenye Biblia ili kupata zaidi.

    1. Mnyama hukusanya nguvu za dini na siasa kwa pamoja, wakamsujudu huyo mnyama....”Ufunuo 13:4.

    2. Mnyama alichukua uongozi katika eneo lisilo kuwa na watu wengi duniani, “Kisha nikaona mnyama akitoka baharini” Ufunuo 13:1.

    3. Mnyama alipata nguvu zake na uwezo kutoka kwa Shetani, hivyo basi tungetarajia historia yake kujumuisha kiasi kikubwa cha udanganyifu, “joka akampa [mnyama] nguzu zake, na kiti chake cha enzi, na uwezo mwingi”Ufunuo 13:2.

    4. Mnyama alitawala kwa ukatili akichukua utawala kamili kwa miaka 1260. Muda huu lazima ulikuwa na pahali wazi pa kuanzia na pa kumalizia na ‘jeraha la mauti’. “Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.” “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti.” “Akapewa uwezo juu ya kila kabila, na jamaa, na lugha, na taifaUfunuo 13:5, 3, 7.

    5. Mnyama aliwatesa Wakristo kwa miaka 1260. “Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda:” Ufunuo 13:7.

    6. Mnyama atapona kabisa kutokana na ‘jeraha la mauti’ na dunia itamstaajabia mnyama yule, “na pigo lake la mauti likapona: dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.”Ufunuo 13:3.

    7. Mnyama ana 666 ya kushangaza ambayo hutambua ofisi yake na jina, “aihesabu hesabu ya mnyama huo: maana ni hesabu ya kibinadamu; na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita”Ufunuo 13:18.

    8. Mnyama ufukuru kwa kudai kuwa yeye ni Mungu na kupeana msamaha (nguvu za kusamehe dhambi za wengine).

    9. Mnyama alifanya madai mengine ya kufukuru, akifanya matendo ambayo ni haki kamili ya Mungu peke yake. “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru”Ufunuo 13:5.

    Msomaji mpendwa , ni nguvu ipi katika historia ambayo inatimiza alama zote za kujitambulisha? Kwa moyo uliyo mkunjufu, kuna jibu moja tu: Kanisa la Kikatoliki la Kirumi. Kanisa la Kikatoliki la Kirumi ndiyo mnyama ambaye Mungu, kwa upendo, anatuonya kuhusu. Si kusudi la nakala hii kushambulia Wakatoliki wa Kirumi, lakini kufunua ukweli kuhusu mpangilio wa Katoliki. Hakuna ye yote ambaye anapaswa kukasirishwa, lakini kuhimidiwa kutafuta ukweli na uhakikisho.

    11. Tafadhali unga mkono hatima hii kwa ushahidi na ukweli.

    Wacha tuchukue kila kitambulisho ili kuona vidokezo vya kihistoria viliopo peke yake katika Kanisa la Kikatoliki la Kirumi.

    1. Kanisa La Kikatoliki la Kirumi huchanganya nguvu za kidini na kisiasa kwa pamoja:

    Mtakatifu Yohana aliona umoja huu katika maono yake ya kinabii kuhusu ufalme wa nne na wa mwisho wa dunia na anaufafanua kama, mwanamke [aliye] keti juu ya mnyama mwekundi sana”Ufunuo 17:3.

    Katika Biblia, mwanamke ni ishara ya kanisa, “kama vile mke amwachavyo mumewe kwa hiani, ndivyo mlivyonitenda mimi kwa hiani, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA.” “Maana…kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi”Yeremia 3:20; Wakorintho wa pili 11:2.

    Kwa kuongezea, inaeleweka kwa kukubaliana katika unabii yakuwa mnyama ni taifa. Hata katika ulimwengu wa sasa, mataifa yanaonyeshwa kama wanyama. Amerika inaonekana kama tai, Urusi inafananishwa na dubu, na China hubeba sanamu ya joka.

    Miaka mingi iliyopita, Munga alimfunulia Danieli falme zote za dunia hadi mwisho wa dari. Katika maono, Danieli aliona mnyama wa mwisho kuwa “mbali na wenziwe wote”Danieli 7:19. lakini inawezake kuwa ya mbali? Kulingana na Ufunuo 17:3, kama inavyo onekana hapo juu, mnyama huyu (taifa) atakuwa na mwanamke (kanisa) akiitawala.

    Je! hivi leo, kuna kanisa na jimbo ambalo linafanya kazi kwa pamoja kama nguvu moja inayotambulikana ulimwenguni kote? Kitu chenyewe haswa duniani ambacho kimekamilisha hii ni Kanisa la Kikatoliki la Kirumi.

    Papa wa Kanisa la Kikatoliki ni kiongozi kamili wa kidini wa zaidi ya wafuasi bilioni moja duniani kote.

    “Pontifa wa Kirumi, kama mridhi wa Petro, ndiye chemichemi ya umilele na inayo onekana na msingi wa umoja wa maaskofu wa kampuni nzima ya waaminifu” Tume ya pili ya Vatikani (1962-65)

    “Kila mshemanzi lazima amtii Papa, hata kama ataamuru kilicho kiovu; kwa kuwa hakuna ye yote ambaye anayeweza kumuhukumu Papa.” Papa Innocent wa tatu (1198-1216)

    Kwa pamoja, papa ni mfalme juu ya taifa huru la Mji wa Vatikani. Vatikani ni taifa ndogo kuu la kitofauti, ijapokuwa ipo kati ya Italiano. Kwa hivyo,upapa ni nguvu za kipekee zinazo changanya udini na nguvu za umma.

    2. Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lilichukua uongozi katika eneo lisilo kuwa na watu wengi duniani:

    Hii inaonyesha vikamilifu Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lilipoinuka katikati ya nguvu tofauti na mataifa ya Uropa.

    3. Historia ya Kanisa la Kikatoliki la Kirumi imejawa na udanganyifu.

    Wakatoliki waliyo fahamishwa uhakikisha udangayifu kama njia ya maisha kwa mapapa. Hans Kung, padri wa Kikatoliki na msomi wa Biblia aliyekuwa mshauri wa Tume ya Pili ya Vatikani (1962-1965), alisema kuwa mapema karne ya tano, mapapa “kwa udanganyifu waliongezea nguvu zao kwa udanganyifu mbaya.”Kanisa la Kikatoliki: Historia Fupi (iliyotafsiriwa na John Bowden), uk. 61

    Moja wapo ya mifano mizuri ni hati ya Tolea la Konstantine, iliyotolewa tarehe 30, Machi, 315 AD, ambayo Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lilibini ili kujiongezea nguvu zake na uwezo. Kupitia hati hii ya uongo, Papa Stefano wa tatu katika karne ya nane alimshawishi Pepini, mfalme wa Wafranki, kuwa majimbo ya Lombadi yalikuwa yamepeanwa na Konstantine kwa Kanisa la Kikatoliki la Kirumi. Hii ilimwongoza Pepini kuwapiga Walombadi na kuteka nyara miji kwa ajili ya papa. Katika 1440, hati hii ilishuhudiwa kuwa ya udanganyifu na msaidizi wa papa aliyeitwa Lorenzo Valla, il hali papa baada ya papa hawakukubali au kukiri udangayifu huu. Hadi wa leo, kuna maandishi katika ndimbwi la ubatizaji la Mtakatifu Yohana Laterani katika Roma ikitunza hati hii ya udanganyifu.

    Papa aita mpangilio mpya wa dunia:

    “MJI WA VATIKANI (AP) – Papa Yohana Paulo wa pili alipiga simu Alhamisi ya Mwaka Mpya na mwito mpya wa …umbaji wa mpangilio mpya wa dunia msingi wake ukiwa juu ya heshima kwa ukuu wa mwanadamu na usawa kati ya mataifa.” Ilitumwa Alhamisi, Januari 1, 2004: 9:21 AM EST (1421 GMT)

    “Jambo kuu ambalo linafunika mpangilio wote wa Mpinga Kristo -- Mpangilio Mpya wa Ulimwengu – ni uongo mtupu. Kwa kweli, waandishi wa Mpangilio Mpya wa Dunia hujigamba kuhusu mpango wao wa udanganyifu, kwasababu kwa ukatili hao uamini kuwa umati mkubwa wa ulimwengu ni wapumbavu sana na wazembe kujua ni nini nzuri kwao. Ni wapangaji tu wa Mpangilio Mpya wa Dunia wanaojua ni nini nzuri kwa ulimwengu, na wameamua kuwa watafikia lengo lao la uongo mtupu kwa watu masikini.” Bill Cooper, “Tazama Farasi Mweupe ” Uk.49

    4. Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lilitawala kwa ukatili kwa miaka 1260 likiwa na utawala juu ya mataifa mengine. Muda huu unapahali wazi pa kuanzia, na ‘jeraha la mauti’ mwishowe:

    Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lilipokea jeraha lake la mauti mnano mwaka wa 1978 wakati [Papa Pius wa nne] alipopelekwa gerezani huko Ufaransa kwa amri ya Napolio.

    “Mnamo mwaka wa 1798 Jenerali Bathaya ilingia Roma, akamaliza serikali ya mapapa, na akaanzisha serikali ya kawaida.” Toleo la 1941 la Encyclopedia Britannica.

    Baada ya kuhakikisha mwisho wa unabii kuwa mwaka wa 1798, tukirudi nyuma miaka 1260, tulifikia 538 AD. Kwa mapapa kutimiza alama hii ya utambulisho, tukio la maana lazima lilitendeka katika 538 AD ilikuweka mwanzo wa muda wa miaka 1260.

    Ushahidi wa kihistoria unafafanua kuwa katika 533 AD Jastini wa Ufalme wa Urumi alitambua ukuu wa kikanisa wa papa kama ‘kichwa’ cha makanisa yote katika falme zote za kusini na magharibi mwa Urumi. Walakini, ilikuwa hadi 538 AD wakati upapa uliachiliwa kabisa kutoka kwa upinzani wao wa Ariani, Wastrogothi (ambao kwa wakati huo walikuwa wakitawala Italiano) ndiyo papa alitokea kama umbo linalo ongoza katika Magharibi. Kwa hivyo, Mnamo 538 AD jukwa liliwekwa la kuendelea kukua kwa kupanda kwa upapa.

    “Vijiliasi...akipanda kiti cha upapa (538 A.D.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisariasi.” Historia ya Kanisa la Kikristo, Toleo la tatu, Uk. 327

    Upapa ukiendelea kuongezeka kinguvu, hakutawala wafuasi wake peke yake lakini pia viongozi na wafalme wa Uropa. Hadi mwisho huo, mapapa walipeana hati kadhaa za kipapa za kusaidia utawala wao dhidi ya wafalme wa Uropa:

    “Ni ofisi ya upapa kutembea chini ya miguu ya wafalme na watawala. J.H. Ignaz Dollinger, Papa na Tume, (London), Uk. 35

    “Ogopa basi, hasira yetu na mgurumo wa kulipisha kwetu; kwa kuwa Yesu Kristo ametuteuwa sisi (mapapa) kwa kinywa chake mwenyewe kuwa wahukumu kamili wa wanadamu wote; na wafalme wenyewe wako chini ya mamlaka yetu.” Papa Nikolasi wa kwanza (858-867 AD)

    Kwenye hati ya upapa ya Papa Gregory wa tisa, iliyoandikwa tarehe 1372 AD, jina lake In Coena Domini, papa alitangaza utawala wa upapa juu ya ulimwengu wote wa Kikristo, wa kidunia na wa kidini, na kuwatoa wote wale waliokataa kutii mapapa na kuwalipa ushuru. Hati hii ya upapa ilihakikishwa na mapapa wengine na, mnamo 1568 AD, Papa Pius wa tano aliapa kuwa itabakia kuwa sheria ya milele.

    Mfano mzuri wa msemo uliyo hapo juu ilikuwa vile Papa Gregory wa saba alivyofanywa mnamo 1077 AD na Mfalme Henry wa nne, Mtawala wa Ujerumani. Wakati mfalme alionekana kupuuza mamlaka ya papa, papa alimtoa na kumtoa uongozini. Henry akaamua kuwa na amani na papa na akavuka milima katika msimu wa baridi ili kujinyenyekesha. Wakati alipofikia jumba la kifahari la papa, Henry alifanywa asubiri ruhusa ya kumuona papa katika uwanja wa nje, mguu mtupu na kichwa chake kama kimefunikwa, na kama amevikwa mavazi yaliyo mabaya. Ilimchukua mfalme siku tatu za kufunga na kuungama kabla papa aweze kumsamehe.

    Hivi leo, madai ya ukuu juu ya viongozi wa ulimwengu unaendelea kushikiliwa na upapa:

    “Muona wa Kwanza [papa wa Roma] haukumiwi na mwingine. Ni haki ya Pontifa wa Kirumi peke yake kuhukumu...wale ambao wanashikilia nyadhifa za juu katika ofisi ya umma katika jimbo... hakuna maombi au mabadiliko dhidi ya uamuzi au tangazo la Pontifa wa Kirumi” Kanuni za Sheria za Kanoni (Tangazo la Paulist,1985), pp. 951, 271

    5. Kanisa La Kikatoliki la Kirumi liliwatesa Wakristo kwa muda wa miaka 1260:

    Kupitia muda huu wa kihistoria (inayojulikana pia kama Miaka ya Katikati), Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lilishikilia usawishi mkubwa Uropa yote, na kila raiya alihitajika awe Mkatoliki wa Kirumi. Kukosa kujitolea kivyo vyote vile kwa papa ingeadhibiwa kwa mateso au kifo. Hii iliongoza mpangilio wa Katoliki la Kirumi kuwa moja wapo ya dini iliyokuwa inatesa sana ambayo dunia imeshawahi kujua, kulingana na Mapadri wa Kristo: Sehemu ya Giza ya upapa, na Petro de Rosa, p. 180

    “Kwa kukiri imani kinyume na Kanisa la Kirumi, historia ilinakili mauaji ya zaidi ya watu milioni mia moja. Mafunzo Mafupi ya Biblia, Uk. 16

    “Lazima tuiwekee kiwango mahakama… kama moja wapo ya kitendo kibaya kabisa kwenye rekodi ya mwanadamu. Will Duranta, hadithi ya Maaendeleo, Toleo la 4, Uk. 78

    “Ya kuwa Kanisa la Kirumi limemwaga damu nyingi isiyo na hatia zaidi ya shirika lingine lo lote ambalo limeshawahi kuwepo kwa mwanadamu hautaulizwa na Protestanti ye yote ambaye anaufahamu kamili wa historia. Ni vigumu kubuni wazo la wingi wa wahasiriwa wake, nani kweli kuwa hakuna nguvu zo zote za kuwaza ambazo zinaweza kungundua kabisa mateso yao.” W. E. H. Leeky, Historia ya Kuinuka na Usawishi wa Roho ya Kufuata akili za kibinadamu katika Uropa, Tolea la 2:32, nakala ya 1910

    Katika Ensyclopidia ya Kikatoliki, Tolea la 12, ukurasa wa 266, msomaji atapata nakala ndefu inayofafanua uwezo wa Kanisa la kikatoliki la Kirumi katika kuwaadhibu ‘wazushi’, Ambao hatia yao ilikuwa kuwa Wakristo waaminifu walio amini Biblia.

    6. Kanisa la Kikatoliki la Kirumi litapona kabisa kutokana na ‘jeraha lake la mauti’ na dunia nzima itastaajabu:

    Wakati Papa Paulo wa nne alipokufa korokoroni huko Ufaransa mnamo 1799, ulimwengu ulitarajia mwisho wa Kanisa la Kikatoliki la Kirumi. Walakini, Mungu alikuwa ametuambia yapata miaka 2000 iliyopita ya kuwa mnyamba atapona kutokana na jeraha lake la mauti. Hivi ndivyo gazeti la New York Times lilivyo ripoti kuponywa kwa mnyama, upapa:

    “JERAHA LA MWANADAMU LAPONA: Roma, Juni 7.-- Kwanzia saa tano asubuhi hii kulikuwa na Jimbo kuu lingine huru ulimwenguni. Wakati huo Mbunge Mkuu Mussolini… alibadilishana na Kadinali Gasparri, Karani wa Jimbo la upapa, akiwakilisha Papa Pius wa nne, akihakikisha makubaliano yaliyo tiwa sahihi katika Nyumba ya kifahari ya Laterani mnamo Februari 11. Kwa kitendo hicho rahisi Jimbo kuu huru la Mji wa Vatikani likatokea.”New York Times, Julai 7, 1929

    Mambo ya nyakati ya San Francisco iliripoti ‘kupona’ kwa upapasi kama ifwatavyo:

    “Mussolini na Gaspari (Kadinali) walitia Sahihi ya Makubaliano ya Kihistoria...Kuponyesha Jeraha la miaka nyingi.” Mambo ya nyakati ya San Francisco, Julai 7, 1929

    Je! Ulimwengu wa sasa ‘unastaajabia’ upapasi, kama vile Biblia ilivyotabiri?

    “Njia nzuri kabisa ya kumuheshimu Yohana Paulo wa pili, kwa kweli mmoja wa watu wakuu, ni kuchukua mafunzo yake kwa umakini, kwa kusikiliza maneno yake na kuweka kwa matendo maneno yake na mafunzo yake hapa Marekani. Huu ni mwito ambao nilazima tuukubali.” Rais George W. Bush, Machi 21, 2001

    Papa yohana Paulo wa pili ni mmoja wa viongozi wadilifu wakuu na wakiroho wa karne hii.” Billy Graham katika Tangazo la Jumamosi Jioni, Jan-Feb. 1980

    “Namtamani Papa Yohana wa kumi na tatu sana. Nahisi kuwa alileta mfumo mpya ulimwenguni”. Billy Graham, Baraza la Chicago, Juni 8, 1963

    “Papa Yohana paulo wa pili husherekea ibada ya nje katika Kiispania kwa watu zaidi ya milioni moja katika Mji wa Mexico.” New York Times, Jan 25, 1999

    “Usiku wa Jumatano wakati Baba Mtakatifu alikuwa akitembea na Makamu wa Rais Gore barabarani ...ili kupanda “Shepherd 1” na kurejea Roma, watu walilia, wakapeperusha vitambaa na kushangilia “Yohana paulo wa pili, tunakupenda!” ... ilikua matembezi mafupi lakini ya kuvuta na ya nguvu na Papa kwa Mtakatifu Louis.” Jan 28, 1999 (Habari za EWT)

    “Hakuna shaka kuwa Paulo wa sita, pamoja na Yohana wa ishirini na tatu na Yohana Paulo wa pili, watakumbukwa kama Mapapa watatu wakuu wa Amani, waanzilishi wa kuendelea kukuu kwa Kanisa la Kikatoliki katika Mwaka Mpya.” Robert Muller, Karani MsaidiziMkuu wa kitambo wa Umoja wa Mataifa

    7. Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lina namba ya kushangaza ya 666:

    Jina rasmi la papa ni “Vicarius Filii Dei”, ambayo ikitafsiriwa ni, “Mwakilishi wa Mwana wa Mungu”. Ili kuhakikisha, gazeti la Kikatoliki Mgeni wetu wa Jumapili la Aprili 18, 1915 iliandikwa: “Maandishi yaliyo andikwa kwenye Kofia ya papa ni kama ifwatavyo: ‘Vicarius Filii Dei’”. Kwa kuwa katika kilatino herufi zingine zina udhamana wa kinambari, tunapaswa tu kuyaongezea yote kwa pamoja ili kupata 666.

    8. Kanisa la Kikatoliki la Kirumi ufukuru kwa kudai kuwa ni Mungu na kupeana msamaha:

    Tunashikilia ulimwenguni sehemu ya Mungu Mkuu.”Papa Leo wa kumi na tatu, katika barua ya makasisi, iliyoandikwa tarehe 20, Juni, 1894

    Papa si tu mwakilishi wa Yesu Kristo, mbali ni Yesu Kristo, akiwa amefichwa chini ya kitambaa cha mwili.” Taifa la Kikatoliki, Julai 1895

    “Lakini mwalimu mkuu kanisani ni Pontifa wa Kirumi... [ambaye] anahitaji ...kunyenyekea kikamilifu na utiifu wa mapenzi ... kama vile Mungu Mwenyewe.”Papa Leo wa kumi na tatu, Barua kuu za makasisi, Uk. 193

    “Inaonekana kuwa Papa Yohana Paulo wa pili sasa anatawala Kanisa duniani kutoka kwa Sehemu Yake juu ya Msalaba wa Kristo.” Ilitolewa kutoka kwa nakala iitwayo, “Kasisi wa Aukland Asema Papa Atawala Kutoka Msalambani” AUCKLAND, Nuzilandi, SEPT. 20, 2004, Zenit.org

    “Kwa kweli, si sana kusema kuwa katika maoni ya ufahari wa ofisi zao, mapadri ni miungu wengi.” Papa Innocent wa tatu

    Kanisa la Kikatoliki la Kirumi liliumba ‘soko’ kubwa duniani la bidhaa za aina tofauti, ambazo hakukuwa na wapinzani na hitaji lisilo kwisha. Alidai kuwa alikuwa na haki ya kuuza neema ya Mungu, kitendo Chake cha huru cha kusamehe, kwa wenye dhambi. Hadi wa sasa, nguvu hii ya kufukuru, inashikilia nguvu za kusamehe dhambi.

    “Uwezo wa mahakama itajumuisha pia nguvu za kusamehe dhambi.” Ensyclopedia ya Kikatoliki, Toleo la 12, -nakala ya “Papa”, Uk. 265

    “Na Mungu mwenyewe inampasa kukubaliana na hukumu ya wakuhani wake na asisamehe au asamehe, kulingana kama wamekataa kupeana msamaha, bora mwenye kuungama anaweza kuifanya.” Heshima na Kazi ya padri, uk. 27, New York Nduguze Benzija, Wachapishaji kwa Utume Mtakatifu, Angalia 1888

    9 Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lilifanya madai mengine ya kufukuru kwa kufanya matendo yanayo muhusu Mungu peke yake:

    Hapa kuna mifano ya madai ya kufukuru na mafunzo ya Kanisa la Kikatoliki la Kirumi:

    “Padri ana nguvu za vifunguo, au nguvu ya kuwakomboa wenye dhambi kutoka jehanamu, ya kuwafanya wastahili paradiso, na kuwabadilisha kutoka kuwa wafungwa wa Shetani hadi kuwa wana wa Mungu. Na Mungu mwenyewe anapaswa kukubaliana na hukumu ya mapadri… Bwana Mkubwa wa ulimwengu anawafwata tuu watumishi kwa kuhakikisha mbinguni yote ambayo waliamua duniani.” Liguori, “Kazi na Heshima ya Padri”, pp. 27, 28

    “Kwa hivyo padri anaweza, kwa njia fulani, kuitwa muumbaji wa Muumbaji wake, kwa kuwa kwa kusema maneno ya kutakasa, anaunda, kama ilivyokuwa, Yesu kwenye Sakramenti, kwa kumpatia kuwapo kwa sakramenti, na kwa kumtoa kama mhasiriwa wa kupeanwa kwa Baba wa milele… Nguvu za padri, ni nguvu za mtu wa milele; kwa kuwa kubadilisha mkate inahitaji nguvu zaidi kama kuumba ulimwengu.” Mtakatifu Bernadine wa Sienna

    “Mapadri ni wakombozi wa dunia.” Mtakatifu Jerome

    Kwa vitendo vyake vya kufukuru, Kanisa la Kikatoliki la Kirumi limetenda kitendo kikubwa zaidi ya zote cha kufukuru. Alibadilisha sheria ile ya Mungu - Amri Kumi. Alijaribu kufutilia mbali amri ya pili yote, kwa kuwa ilikemea mafunzo yake na tamaduni. Na mbaya zaidi, alibadilisha siku ya kuabudu kwenye Amri ya Nne kutoka Jumamosi hadi Jumapili. Hii ilifanywa ijapokuwa Mungu alimpa Adamu amri hii ya milele wakati wa uumbaji na ametuhakikishia kuwa “Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu”Zaburi 89:34.

    Amri Kumi ndizo sehemu peke yake ya Biblia ambayo ilibadilishwa na sauti ya Mungu katika uwepo wa kongamano. Na kuhakikisha kuwa Musa hakukosa herufi hata moja, Mungu aliziandika kwa kidole Chake na akampa Musa. “Haya ndiyo maneno ambayo [Sheria kumi] Bwana aliwaambia mkutano wenu wote…wala hakuongezea neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe…”Kumbukumbu 5:22

    Kristo anasisitiza zaidi kutokubadilishwa kwa Amri Kumi wakati aliposema, “lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke,kuliko itanguke nukta moja ya torati”Luka 16:17. Jua ikingaa mbinguni, dunia ngumu unayoishi, ni washahidi wa Mungu ya kuwa sheria Yake haiwezi kubadilika naniya milele. Ijapokuwa zinaweza kupita, mafunzo yake ya milele yatavumilia. Kristo alihakikisha zaidi “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati, au manabii: la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana,amini, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie”Mathayo 5:17, 18.

    Kanisa la Kikatoliki halina aibu yakuwa ilibadilisha siku ya kuabudu. Kwa kweli, anajivunia katika kitendo hiki, na uionelea kama ‘alama’ yake ya uwezo na ukubwa juu ya makanisa mengine na dini.

    “Sabato,siku iliyojulikana vizuri ya torati, ilibadilishwa kuwa siku ya Bwana. Hii na zingine hazijakoma kwasababu ya maagizo yaliyopokewa kutoka kwa Kristo, (kwasababu yeye mwenyewe alisema, sijakuja kuitangua torati, lakini kuitimiliza), lakini kwasababu ya mamlaka ya kanisa zimebadilishwa.” Askofu mkuu wa Rheggio, Ujumbe wa 1-18-1562, Mansi XXIII, Uk. 526

    “Jumapili ni shirika la Kikatoliki, na madai yake ya utakatifu yanaweza kutetewa kwa mamlaka ya Kikatoliki peke yake... Katika Maandiko Matakatifu kuanzia mwanzo hadi mwisho hatupati andiko hata moja ambalo linasawazisha ubadiliko huo wa ibada ya kuabudu ya umma kila wiki kutoka siku ya mwisho hadi siku ya kwanza ya wiki.” Matangazo ya Kikatoliki, Sidney, 8-25-1900

    “Hakuna po pote kwenye biblia ambapo imeandikwa kuwa ibada inapaswa kubadilishwa kutoka Jumamosi hadi Jumapili. Ukweli ni kuwa Kanisa lilikuwepo kwa karne kadhaa kabla Biblia haijapeanwa duniani.Kanisa ilitengeneza Biblia; Biblia haikutengeneza Kanisa.” Mambo ambayo Wakatoliki wanaulizwa Kuhusu, na Martin j. Schott, 1927 ed, uk. 136

    “Tunasherekea Jumapili badala ya Jumamosi, kwasababu Kanisa la Kikatoliki lilibadilisha utakatifu kutoka Jumamosi hadi Jumapili kwenye baraza la Laodikia mnamo mwaka wa 364 AD.” Mafunzo ya Kitabu cha Waumini cha Katoliki, kutoka p. Geiermann, kazi ya Papa Pius wa kumi, mnano 1-25-1910

    Kulingana na Kanisa la Kikatoliki la Kirumi ‘Jumapili’ ni alama yao ya siri na ya kitofauti ya uwezo.

    “Jumapili ni alama yetu ya uwezo. Kanisa liko juu ya Biblia, na ubadilishanaji huu wa kuzingatia Sabato ni udhibitisho wa ukweli.” Rekodi za kikatoliki, London, Ontaria, Septemba 1,1923

    Waprotestanti Kuzingatia Jumapili ni heshima wanao toa, haijalishi hao wenyewe, kwa uwezo wa Kanisa (Katoliki), Mazungumzo ya Kawaida Kuhusu Waprotestanti wa Kisasa, na Monsignor Segur, uk. 213

    “Lakini akili ya Mprotestanti inaonekana kutofahamu kuwa katika ... kuzingatia Jumapili. . . wanakubali uwezo wa mnenaji wa kanisa, papa.” Mgeni Wetu wa Jumapili, Nakala ya Kila Wiki ya Kikatoliki, Feb. 5, 1950

    “Kwa kweli Kanisa la Kikatoliki linadai kuwa ubadiliko huo ni kitendo chake… alama ya nguvu yake ya kanisa na uwezo

    katika mambo ya kidini.” Ofisi ya Kadinali Gibbons, Kupitia Mshauri mkuu C.F. Thomas, Nov 11, 1895

    Kutoka kwa ushahidi mkuu mzito, tunaweza kutamatisha kwa kukubaliana kuwa mnyama wa Ufunua mlango wa 13 na 14 ni Kanisa la Kikatoliki la Kirumi, na kuwa alama yake (alama ya mnyama) ni kuzingatia Jumapili.

    Je! Ni kwanini alama hii niya maana sana? Je! Umeshawahi kutia sahihi hati ili kuifanyiza au kuhakikisha ukweli wake? Je! Umeshawahi kupeana ‘muhuri wako wa kukubali’ kitu fulani? Ni lazima katika serikali yo yote. Kwa kutia sahihi peke yake, hati inakubalika. Makubaliano ya serikali lazima kila wakati yawe na alama rasmi au muhuri. Je! alama au mihuri ya serikali ina mambo gani? Muhuri rasmi au sahihi lazima ijumuishe mambo matatu:

    • Jina la mkubwa
    • Cheo cha mkubwa
    • jimbo au sehemu ya utawala wake

    Kwa mfano, wakati Rais wa Marekani anapo tia sahihi mswada kuwa sheria, lazima atie sahihi, George Washington (jina), Rais (cheo) wa Marekani (jimbo). Kila hati lazima itiwe sahihi katika mpangilio huu ili iwe rasmi na halali.

    Tukimwangalia Muumbaji Mkuu, tunagundua kuwa ana Ufalme wa Mbinguni. Na hati inayojumuisha torati ya Ufalme Wake ni Amri Kumi. Ukiangalia sambamba katikati yao utapata muhuri ya Mungu anayeishi! “Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, na bahari..” Kutoka 20:11.

    Gundua mambo matatu tofauti:

    • Jina: BWANA (“ mimi ndimi Bwana: hilo ndilo jina languIsaya 42:8)
    • Cheo: MUUMBAJI ( “BWANA alifanya”)
    • Jimbo: MBINGU NA NCHI ( “Mbingu na nchi”)

    Wazi wazi, muhuri wa Mumbaji unapatikana katika amri ya Sabato ya Torati Yake. Ni kugundua uwezo Wake kama Muumbaji. Tunapo itunza Sabato Yake, tunaonyesha kuwa tunamgundua Yeye kama Muumbaji wetu.

    Nafasi ya kumuabudu Mungu kama Muumbaji wetu. Tunapoiweka siku ambayo Bwana aliichagua takatifu, tunatangaza duniani kote kuwa Muumbaji wa ulimwengu ni Mungu wetu! Ibilisi, “Lusifa” anashambulia Sabato, kwasababu anataka aabudiwe “kama Yeye aliye juu”Isaya 14:14. Muumbaji anatafuta ibada yako katika siku Yake takatifu ya Sabato, na Shetani, akitafuta kuwa kama Muumbaji, anataka ibada yako Jumapili yake. Je! Utachagua ipi?

    “Zitakaseni sabato zangu; nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.” Ezekieli 20:20.

    Kuitambua Sanamu ya Mnyama

    12. Kwa hivyo basi Sanamu ya mnyamba ni ipi, ambayo Mungu anatuonya tusiiabudu?

    Ili kuweza kutambua sanamu ya mnyama, tunapaswa kwanza tutambue mnyama aliye na pembe mbili ambayo itasaidia katika kuunda sanamu ya mnyama:

    “Kisha nikaona mnyama mwingine akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikluwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. 12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake, naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona... 14 ...akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama,aliyekuwa na jeraha la upanga, naye akaishi. 15 akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. 16 Naye akawafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: 17 Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufunuo 13:11-12, 14-17.

    Mnyama huyu mwenye pembe mbili ana alama zifwatazo za kutambua:

    1. Mnyama huyu alitokea wakati upapa ulipokea jeraha lake la mauti mnano mwaka wa 1798, “mnyama mwingine akipanda juu” Ufunuo 13: 11.

    2. Mnyama huyu alipanda juu kutoka duniani, kinyume na mnyama wa kwanza aliyepanda juu kutoka baharini. Kama ‘bahari’ inawakilisha watu wengi na mataifa, basi ‘inchi’ inawakilisha eneo lililo na watu wachache. Kwa hivyo, taifa hili lingeinuka kutawala katika eneo lililo na wakazi wachache.

    3. Mnyama huyu ana pembe mbili zilizo kama mwana-kondoo. kulingana na Biblia, pembe uwakilisha uweza. “Alikuwa na pembe…ndipo ulipofichwa uweza wake” Habakuki 3:4. Kwa hivyo, taifa hili lina uweza mara mbili mbali mbali, tofauti na ile nyingine. Pia, mwana-kondoo ni ishara ya Kristo; hivyo basi, tunaweza amua kuwa taifa hili lilianzilishwa kwenye kanuni safi na nzuri za Kikristo.

    4. Walakini, mnyama huyu huzungumza kama joka; taifa ‘unena’ kupitia uweza wa wana sheria au mahakama. ‘pembe kama mwana-kondoo’ na ‘sauti ya joka’ inadokeza utofauti mkubwa kati ya kazi za amani na mafunzo ya taifa hili.

    Msomaji mpendwa , tena tunauliza, ni taifa lipi linalo timiliza alama hizi za utambulisho? Kuna jibu moja: Marekani.

    1.Marekani ilitokea kuwadia mwaka wa 1798: Kulikuwa na taifa moja tu ambalo liliinuka wakati huo upapa ulikuwa ukipoteza nguvu mnano mwaka wa 1798. Unabii huu unadokeza sambamba Marekani. Marekani ilitungwa chini ya Katiba kama serikali ya muungano mnamo mwaka wa 1787.

    2.Marekani iliinuka katika ardhi isiyo kuwa na watu wengi: Marekani haikukua katika Ulimwengu wa Kitambo ambao ulijawa na wingi wa makutano, lakini katika Ulimwengu Mpya, ambao una wakazi wachache kiasi.

    3.Marekani ina uwezo mara mbili mbali mbali ambayo msingi wake uko kwenye kanuni za Kikristo. Marekani ina serikali ya kipekee, ambapo kanisa na jimbo ufurahiya uhuru unao peanwa na Katiba. Kwasababu ya mfumo huu wa serikali, Marekani kwa kweli ni Jamhuri (ufalme bila mfalme) na Protestanti (kanisa bila papa), na nguvu zao zote zikiwa zimegawanyishwa. pia, hali yake ya kuwa kama mwana-kondoo ilifanya Marekani kimbilio kwa waliyoteswa na kufinyiliwa wa mataifa mengi.

    “Muumbaji anatafuta ibada yako kwenye siku Yake ya Sabato, na Shetani, akitafuta kuwa kama Muumbaji, anataka ibada yako Jumapili yake. Je! Utachagua ipi?”

    4.Marekani uzungumza kama joka: Torati ya Marekani ya maana sana iliyoandikwa katika katiba yake inahakikisha uhuru wa mawazo wa kila mmoja . Hakuna cho chote ambacho kimependwa au cha maana zaidi. Walakini, Marekani tayari imeshaanza na hivi karibu itakataa vikamilifu kila kanuni ya Katiba yake. Na kile ambacho kinapeana umaana mkubwa kwa mfumo huu ni ukweli wakuwa jambo la maana ni kutiliwa mkazo kwa kuzingatia Jumapili.

    kitendo hiki kitakuwa kinyume sambamba na kanuni za serikali hii, kwa wenye akili wa shirika lake la bure, kwa Ukubaliano wa Uhuru, na kwa Katiba. Katiba usema kuwa “Baraza kuu halitafanya sheria yo yote ya kupendelea uwanzilisho wa dini, au kuzuiya uhuru wake,” na kuwa “hakuna mtihani wa kidini ambao utahitajika kama hetimu ya ofisi yo yote ya umma Marekani.”

    Upinzani wa kitendo kama hicho si kubwa zaida ya vile ilivyoonyeshwa kwenye ishara. Ni mnyama aliye na pembe kama za mwana-kondoo - kikazi ni msafi na bila mawaa – ambaye uzungumza kama joka. Ukizingatia yale yanayotokea katika habari na hapo awali itahakikisha ufafanuzi huu wa kibiblia.

    “Na nina unga mkono vikamilifu kitendo ambacho msingi wake upo kwa imani ambayo tunadokeza, kwasababu siamini kuwa inapinga laini kati ya utengano kati ya kanisa na jimbo, na nina amini kuwa itafanya Marekani kuwa mahali pazuri.” George W. Bush, akifanya mwelekezo uliyochanganyikiwa wa nakala ya Uanzilishi, iliyodokezwa kutoka kwa HABARI za AA #889 za Conrad Goeringer, (Februari 28, 2001) kutoka kwa Wmarekani wasio sadiki . Msemo huu unashambulia Haki ya Mswada wa Katiba ambao unazuiya serikali yetu “kupendelea uanzilisha wa kidini.”

    “Jambo letu la kwanza ni imani yetu.”
    George W. Bush, Greensboro, Carolina ya Kaskazini, Octoba Vidokezo 10,2000 kutoka kwa Jacob Weinberg, “Ubushi Kamili”

    “Ujumbe wa wazi uliyosemwa na usimamizi mpya ni kuwa, Amerika ya George W. Bush ni taifa la Kikristo na kuwa wasiyo-Wakristo wamekaribishwa hemani iwapo watakubali kuitikia hali yao kama wachache waliyo ruhusiwa badala ya kuwa raiya sawa kamili.” Alan M. Dershowitz, katika “Bush aanza kwa kupinga Katiba,” Los Angeles Times, Januari 24, 2001  

    Unabii wakaribia Kukamilishwa hivi karibuni

    13. Ni wazi kuwa mnyama aliye na pembe mbili ni Amerika. Lakini ni uhusiano upi kati ya Amerika na sanamu ya mnyama?

    Ijapokuwa Amerika ilianzilishwa kwenye kanuni zilizo pinga upapa, hivi leo tunaangalia vile Amerika na Vatikani wanafanya kazi karibu sana kwa pamoja ili kufanya usawishi wao uwe zaidi. Biblia inatuambia kuwa siku moja, siyo umilele wa mbali sana, Amerika itapitisha sheria ambayo itawahitaji raiya wake, halafu ulimwengu, kumuabudu mnyama wa kwanza, papa. “Naye [Amerika] atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake[upapa], naye aifanya dunia [kwanza Amerika, halufu dunia nzima] na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza [kuheshimu Jumapili ya upapa] , ambaye jeraha lake la mauti [1798] lilipona [1929] ... akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama [kuiga upapa alipotumia nguvu za umma kulazimisha mafunzo ya kidini] ,aliyekuwa na jeraha la upanga, naye akaishi.” Ufunuo 13:12, 14.

    Hivi karibuni Amerika itakataa uhuru wake wa kidini ili kulazimisha Jumapili izingatiwe (alama ya mnyama). Hii inamaanisha,Makanisa ya kiprotestanti yatatawala serikali ili kutimiza agenda yao. Wakati hii itatendeka, Amerika itakuwa imefanya sanamu kwa Kanisa la Kikatoliki la Kirumi, kuunganisha kanisa na jimbo. Halafu Amerika itazungumza “kama joka” na kutumia “nguvu zote za mnyama wa kwanza”Ufunuo 13:11, 12; atakuwa na roho sawa ya kutovumilia na kutesa ambayo ilidhihirishwa na mnyama wa kwanza, upapa.

    Kwa hivyo, wakati uhuru wa kidini ukipotea,wachache walio kataa hawataepuka mateso, na kutakuwa na marudio ya kutovumilia ya dini ya Umri wa Kati: “Na alikuwa na uwezo wa kupea uhai sanamu ya mnyama [sheria za Jumapili zilizo amuriwa] … na kusababisha kuwa, wengi ambao hawatasujudia sanamu ya mnyama [kwa kupendelea Jumamosi, siyo Jumapili] watauliwa. Naye akawafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, [wale ambao wanapendelea Sabato ya kweli watazuiliwa kununua na kuuza], yaani, jina la mnyama yule…”Ufunuo 13:15-17

    Wengine watapokea alama “katika kipaji cha nyuso zao” kwasababu walichagua “kuamini uongo”Wathesalonike wa pili 2:11. Wengine, ijapokuwa wamesawishiwa kuwa Jumapili siyo Sabato ya kweli, watakubali ili kutunza maisha yao, hivyo basi watapokea alama “katika mkono wao wa kuume” hiyo ndiyo ishara ya kazi.

    14. Ili hii iwe kweli, kunapaswa kuwa na ushahidi wa kuwa kwa sasa upapa unafuata kuinua Jumapili katika Amerika, na kuwa Waprotestanti wa Marekani (maadui wa kihistoria wa Roma), wamebadilisha hisia zao, na wanaonyesha kuwa tayari kushirikiana ili kupitisha sheria za Jumapili. Je! Kuna ushahidi kama huo?

    Hivi wa leo Waprotestanti wengi wanaonyesha upendeleo kuwadia upapa, na hii imehimiza upapa kutafuta kwa bidii kupitisha kuzingatia Jumapili:

    “WaMarekani wote watafanya vyema kumuomba Rais na Baraza kuu kufanya sheria ya Muungano – marekebisho kwa katiba kama itahitajikana – ili kuanzisha tena Sabato (ya uwongo) kama Siku ya kitaifa ya Kupumzika.” MVIRINGO WA MAPACHA YA KATOLIKI, Agosti 25, 1985, “Nakala ya Jumapili”

    “Katika swala hili, aliyenitangulia Papa Leo wa kumi na tatu …alizungumza kuhusu mapumziko ya Jumapili kama haki ya mfanya kazi ambayo Jimbo lazima ihakikishe.” Papa Yohana Paulo wa Pili -AKUFA DOMINI, MEI 31, 1998

    “Kwahivyo… Wakristo kwa kawaida watangangana kuhakikisha kuwa upitishaji wa sheria za umma inapendelea kazi yao ya kuweka Jumapili takatifu. Katika hali yo yote, wanasababishwa kimafikira kupanga mapumziko yao ya Jumapili katika njia ambayo itawaruhusu kushiriki katika Ekaristi, wakiepuka kazi na shughuli ambazo haziambatani na utakaso wa Siku ya Bwana…” Papa Johana Paulo wa Pili, AKUFA DOMINI, Mei 31, 1998

    “…Wakristo [kila mahali] wanapaswa kutafuta kutambua Jumapili na siku takatifu za kanisa kama siku za mapumziko halali.” Kitabu cha Kanisa la Katoliki, toleo maarufu na kamili, 2000, par 2188

    Viongozi wengi wa Protestanti katika Amerika wako tayari kuzika shoka na Wakatoliki:

    “Wakubwa wa Waprotetestanti wa Amerika na makanisa ya Imani ya kusini ambao walipatana na Papa Yohana Paulo wa Pili Alhamisi,walisifu mazungumzo yao ya kwanza iliyowakilishwa kwa upana kama alama ya barabara ya umoja mkumbwa… kasisi Donald Jones, Mmethodisti na mwenye kiti wa idara ya mafunzo ya kidini ya shule ya upili ya Carolina ya Kusini, alisema, ‘mkutano wa maana sana wa kidini wa karne hii.’ Kasisi Paulo A. Crow mdogo, wa Indianapolis, afisa wa dini wa kanisa la Kikristo (Wafuasi wa Kristo), aliita ‘siku njema katika dini’ akifungua usoni ambao Mungu ‘anatuvuta sisi sote pamoja.’” Tangazo la Montgomery, Sept 12, 1987

    Billy Graham :Nimepata kuwa imani yangu ni sawa na ile ya Imani ya Katoliki ya kirumi.” McCall’s, Januari 1978. Pia yeye, alimwita Papa Yohana wa Pili: “Kiongozi mkuu wa kidini wa dunia ya kisasa.” Tangazo la Jumamosi jioni, Januari – Februari 1980

    Paul Crouch : “Ninatoa neno protestanti kutoka kwa matamshi yangu. ... si pingi cho chote… [Ni] wakati wa Wakatolini na wasio- Wakatoliki waje pamoja kama kitu kimoja katika Roho na kitu kimoja katika Bwana.” Kipindi cha “Msifu Bwana”,Trinity Broadcasting Network, Oct 17, 1989

    Robert Schuller : “Ni wakati wa Waprotestanti kumuendea mchungaji [papa] na kusema, “Je! ni nini ambacho tunapaswa kufanya ili turudi nyumbani?”” Mkaguajii wa Herald ya Los Angeles, Septemba 19, 1987, Ukurasa wa dini

    David Wells : “Kama Ukatoliki utakuwa Ukatoliki zaidi usoni, ambayo ndiyo natarajia chini ya papa wa sasa, basi utofauti wa mafunzo ya kibiblia itakuwa kali, lakini ushirikiano na Wakatoliki dhidi ya tamaduni ya kidunia inaweza kua ndani zaidi. mimi, niko tayari kubadilishana.” Gazeti la Umilele, Sept. 1987

    J. L. Packer : “Mafunzo ya kidini ya Waprotestanti na Wakatoliki kuhusu maisha ya Wakristo tarajio lake lote na makusudi yanafwanana. Si hii ni ya maana kwa maisha ya usoni ya Wakristo?” J. I. Packer, Ukristo wa Leo, Juni 22, 1992

    Neal C. Wilson : “Ijapokuwa ni kweli kuwa kulikuwa na wakati katika maisha ya Kanisa la Kiadventisti ya siku ya Saba wakati dini ilichugua maoni kinyume na Katoliki ya Kirumi … hisia… sasa zimetumwa kwenye biwi la takataka la historia kama vile Kanisa la Kiadventisti ya Siku ya Saba inavyohusika.” Neal C. Wilson , Rais wa hapo awali wa Mkutani wa Kawaida wa Adventisti ya siku ya Saba , 1974

    Jinsi ya Kuepuka Chapa ya Mnyama

    15. Hivyo basi, nawezaje kuepuka kupokea chapa ya mnyama?

    Hii ndiyo swali la maana kabisa. Mungu, katika upendo Wake usiyo na kikomo, ametuonya tusimuabudu mnyama na baadaye tupokee chapa yake. Wale ambao wanapokea chapa ya mnyama “watakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Muingu, iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji [bila huruma] katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti…hao wamsujuduo huyo mnyama[kupendelea upapa kupitia kuzingatia Jumapili] na sanamu yake [Marekani ikilazimisha kuzingatia Jumapili] , na kila aipokeaye chapa ya jina lake”Ufunuo 14:10, 11.

    Haya ni maneno ya kutuliza moyo kutoka kwa Mungu Hasira Yake ni sawa na makosa Kwa kupendelea Jumapili, iliyoanzishwa na Shetani kupitia upapa, unatayarisha kupokea chapa ya mnyama.Shetani anataka kuwapotosha wengi awezavyo ili waweze kupendelea siku hii ya kuiga. Ili kukamilisha uongo wake, alichagua Jumapili, siku ambayo Kristo alifufuka akijua kuwa watu wengu wataamini kuwa kuzingatia Jumapili ni vyema kuliko Jumamosi, kwa kuwa inasujudu kufufuka kwa Kristo. Lakini njia moja tu ya kutopokea chapa ya mnyama ni kukataa kusujudu siku ambayo haikuchaguliwa na Mungu. Siku ile tu ambayo Mungu aliiteua kama takatifu ni Sabato ya Jumamosi na kwa kuisujudu utapokea “muhuri ya Mungu anayeishi”Ufunuo 7:2.

    Ukitaka kusujudu kifo na kufufuka kwa Kristo, Biblia wazi wazi inasema unafanya hivyo kwa kubatizwa (kutumbukizwa kabisa). Angalia Warumi 6:3-5. Kwa kuingia ndani ya maji (kuzikwa) unakubali kifo Chake. Kwa kutoka nje ya maji (kufufuka) unakubali kufufuka Kwake.

    16. Je kuhusu mabilioni ya Wakristo wa zamani ambao walisujudu Jumapili badala ya Jumamosi –walipokea chapa ya mnyama bila kujua? Na kuhusu Wakristo wa hivi leo ambao kwa uaminifu udhania Jumapili ni Sabato ya Biblia?

    Wakristo wengi wa kizazi cha zamani walizingatia Jumapili, wakidhania kuwa walikuwa wakiweka Sabato ya Biblia; na hivi leo kuna Wakristo wa kweli katika kila kanisa, ikijumuisha Kanisa la Kikatoliki la Kirumi, ambao wanaamini kuwa Jumapili ni Siku ya Bwana. Hakuna ye yote anayeweza kuulizwa maswali kwa makosa yao kwa kuwa mwangaza haujaletwa kwao. Kwa kuwa Bwana “ukonyeza” wakati wetu wa kupuuza. Angalia Matendo 17:30. Tunahukumiwa peke yake na mwangaza ambao tulikuwa na nafasi ya kuupokea. Lakini, wakati sheria ya Jumapili ya dunia nzima ikipitishwa, swala litakuwa wazi mbele ya wote, na hapo ye yote ambaye atavunja amri ya Mungu, ya kutii funzo ambalo halina mamlaka ya juu izidiyo ile ya Roma, atapokea chapa ya mnyama.

    Hivi karibuni, kila mtu atakabiliana na mtihani huu wa hatari ya milele, kuweka amri za Mungu au za upapa. Je! Utasimama wapi?

    Hakuna Nafasi ya kuwa Fugufugu

    17. Je! Kwanini nijali, kwanini nisiwaachie watu wa kidini watatue?

    Onyo la Mungu la kutuliza moyo katika Ufunuo 14 haiwachi nafasi ya kutofautiana. Yesu alisema, “Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu”Luka 11:23. Mungu uwahesabu watu wote kuwa wameamua ukweli au kinyume chake. Onyo hili halipendelei mtu, kiwango, hali, au dini. Inawahutubia wanadamu wote.

    Siyo lazima sisi kwa kutaka tuchague ufalme wa giza ndiposa tuje chini ya utawala wake. Tunapaswa tu tupuuze kujiusisha wenyewe na ufalme wa mwangaza. Hakuna cho chote ambacho kinahusikana na maslahi ya mioyo ambayo inapaswa kuchukuliwa kwa kutokujali. Mungu ukataa kutokujali katika hoja za kidini.

    Je! Lazima Nifanye nini?

    Kwa kuwa ufugufugu haukubaliwi na Mungu, na tukijua kuwa ili kuepuka kupokea chapa ya mnyama. Lazima nisujudu Jumamosi hata wakati Jumapili imewekwa na sheria na hukumu ya kifo:

    18. Katika hatua za kweli, hatua yangu ya kwanza inapaswa kuwa vipi baada ya kupokea yaliyo hapo juu?

    Mungu anahamu kuu ya kuingia katika uhusiani na wewe. Kwa kweli, Anakutaka uwe mwanawe wa kiume au wa kike. Fikiria fursa ambayo utakua nayo kufanyika mwana wa kiume au wa kike wa Mfalme wa Wafalme, na Bwana wa Mabwana. Nafasi hii ya halali imepeanwa kwako, anakusuburi kwa hamu ili akupe madaraka haya ya juu. Il hali, neno Lake kwako ni, “Msifungwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa: kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Baliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha, 18 Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na kike,asema Bwana Mwenyezi. 7:1 Basi wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu” Wakorintho wa pili 6:14-18; 7:1.

    Kifungu cha maana cha Biblia kinajumuisha kanuni zifwatazo:

    1. Mungu haruhusu kuchanganywa kwa ukweli na makosa (hata kama ni asilimia 99 ukweli). Ni Shetani peke yake ambaye huchanga ukweli na makosa ili kukamilisha uwongo wake. Kwa hivyo, mfumo wo wote wa kidini ambao unajumuisha makosa (kama vile Jumapili kuwa Siku ya Bwana) pamoja na ukweli si wakutoka kwa Mungu. Kwa kuwa “pana shirika gani kati ya nuru na giza?” “Mungu ni nuru,wala giza lo lote hamna ndani yake”Wakorintho wa pili 6:14; Yohana wa kwanza 1:5. Ukweli ni asilimia 100 ama si kweli. Hakuna nafasi ya mafunzo au tamaduni iliyo undwa na mwanadamu.

    “Mgawanyiko unawakilisha hatua ya kwanza ya kweli ambayo unaweza kuchukua ili kuwa mwana wa Mungu”

    2. Kazi ya mtu anayetaka kuwa sawa na Mungu si kuwa mshirika wa kanisa lo lote au mfumo wa dini ambao umejengwa kwa misingi ya Shetani. Mchanganyiko wa ukweli na makosa Mgawanyiko huu unawakilisha hatua ya kwanza ya kweli ambayo unaweza kuchukua ili kuwa mwana wa Mungu, na kufurahiya ndani Yake kama Baba yako.

    tunapo gawanyika, tunaweza kuwa wana wa kiume na wa kike wa Mungu. Kwa kuwa tumeonyesha kuelewa kuwa kuna mifumo miwili peke yake ya kidini katika dunia: Ya Mungu na ya Shetani, na kwa hivyo tumechagua kukata uunganisho wo wote ambao unatuunganisha sisi na mfumo wa kidini uliyo anzilishwa na Shetani.

    3. Tukijua kuwa ukiacha mfumo wa kidini wa Shetani, unapoteza marafiki, jamii, usawishi, kazi, na zingine nyingi …Mungu anakuhakikishia: “ MIMI ni Mwenyezi.” Inamaanisha kuwa atakurudishia zaidi yale yote ambayo utakuwa umepoteza. Yesu anakuahidi: “Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, Ila atapewa mara miasasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele”Marko 10:29,30.

    4. Baada ya kutoka kwa mfumo wa Shetani wa dini, Bwana atatuongoza kwa usawishi wa Roho Mtakatifu ili kutuosha na kuteweka kutokana na dhambi, mawasiliano hayo yanaweza kufunguliwa kati ya Mungu na mwanadamu. Walakini, Mungu anatamani sisi tumtii na kumtumikia, si kwa lazima, mbali kwa kutaka. Msingi wa dini ni upendo kwa Mungu kwasababu ya shukurani kwa yale Aliyotenda ili kufanya msamaha huu uwezekane. Kujiusisha katika huduma Yake kwa tumaini la kulipwa au uwoga wa kuhukumiwa hakuta fanya kitu cho chote.

     

    Upatanisho na Mungu

    19. Je! Ni nini ‘upatanisho na Mungu’, nani kwanini kuna haja yake?

    Wakati Mungu alipo muumba Adamu na Hawa, Walikuwa kamili kitabia na kihisia, na waliishi kwa kutii sheria ya Mungu. Ili kuifanya kawaida kwao kumtii, Mungu aliweka chapa mioyoni mwao za Amri Kumi. Pia aliwafunulia kuwa wakivunja sheria Yake watahukumiwa kwa kifo. “Mshahara wa dhambi ni mauti”Warumi 6:23. Serikali zote zinahitaji sheria safi na hukumu iliyo fafanuliwa vyema kwa wanao vunja sheria hizi. Hebu fikiri hali ya dunia kama adhabu zingesamehewa. Je! Tungekuwa salama kuishi katika mahali ambapo wavunja sheria hawahukumiwi kifungo?

    Wakati Mungu aliwaonyesha Adamu na Hawa sheria Yake, na akaifanya iwe kawaida kwao kuitii kwa kuichapisha mioyoni mwao. Hakutoauhuru wao wa kuchagua. Mungu anaweza kuwa alimuumba mwanadamu bila nguvu za kuvunja sheria Yake; lakini katika hali hiyo mwanadamu hangekuwa chombo adilifu kilicho huru, mbali mashine ya kawaida. Bila uhuru wa kuchagua, utiifu wake haungekuwa wa kujitolea, mbali wa kulazimishwa.

    Kwa kujuta, Adamu na Hawa kwa kutaka waliamua kutokumtii Mungu, ndiposa dhambi ikatengeneza kizuizi kati ya mwanadamu na Mungu. Wakakuwa swala la hukumu ya kifo kwa kuvunja sheria ya Mungu. iliwabidi wafe. Zaidi, hisia safi walizo kuwa nazo za kumtii Mungu zilifisadiwa baada ya kuchagua kutotii sheria Yake. Mioyo yao ilikuwa imepata upinzani na mazoeya ya kutotii.

    Akikabiliwa na makosa ya Adamu na Hawa, Mungu wetu mpendwa angefanya nini? Awaache wote wafe kwa kuvunja sheria Yake? Je! Wazazi wapendwa wa dunia uwaacha watoto wao baada ya hao kuchagua kutokuwatii? au mbaya zaidi, atatoa hukumu ya makosa yao ili kuwakubali? Je! Serikali ya dunia au ya mbinguni, inaweza kuvumilia na kufanikiwa bila hukumu zilizo fafanuliwa vizuri? Kwa kweli haiwezi.

    Kwa ufupi, kama Adamu na Hawa walikuwa walipia makosa yao hao wenyewe, matokeo yake ingekuwa mwisho wa kizazi cha mwanadamu. Au kama Mungu angekuwa aumbe Adamu na Hawa mwingine, hakungekuwa na uhakikisho kuwa hawangechagua kutokutii, kama wenzio waliyo tangulia, na hali hiyo ingefanyika tena. Ni kweli kuwa suluhisho la nje (nje ya eneo la wenye dhambi) lingepangwa. Mpango huu wa mbinguni uliandaliwa na Mungu kitambo kabla ya haja yake kutokea.

    Biblia inasema “siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake”Wakolosai 1:26. Mpango wa Mungu ulijumuisha suluhisho la kurejesha kizazi cha mwanadamu pamoja na Yeye, bila kufinyilia sheria Yake, au serikali kwasababu hata kama Mungu anachukia dhambi, Anampenda mwenye dhambi.

    Suluhisho hili linamaanisha kuwa mtu mwingine asiye na hatia lazima angelipia hukumu ya kifo; hivyo basi, kifo chake kingekuwa kwa bayana ya wenye dhambi. Kwa kifo chake, wenye dhambi waliyo amini watapatanishwa na Mungu, kana kwamba hawakuwa wametenda dhambi, na hivyo haki ya Mungu na upendo wa kizazi cha mwanadamu hakitazozana na kile kingine. Bila kulipia adhabu, hakungekuwa na upatanisho kati ya mwanadamu na Mungu. Na upatanisho unahitajikana ili kuwa sawa na Mungu na kuishi na Yeye mbinguni milele.

    Kwa kuongezea, mtu huyu wa nje ambaye alikuwa afe kwa bayana ya wenye dhambi ndiposa amuonyeshe mwanadamu jinsi ya kuishi ulimwenguni bila kutenda dhambi, ili kuwe na upatanisho dhabiti na Mungu. Je! Kuna haja gani ya kupatanishwa alafu kuanguka nyuma dhambini tena, na kuhitaji tena kupatanishwa? Kwa kawaida, mpango wa Mungu unajumuisha njia ya kumtia nguvu mwanadamu aisha kwa ushindi juu ya dhambi! Ndiposa, ijapokuwa kwa kuvunja sheria ya Mungu, Adamu alipoteza paradiso, katika kutii sheria ya Baba na kupitia imani katika damu inayo samehe ya mtu huu wa nje, paradiso inaweza kupatikana tena.

    20. Nataka kupatanishwa na Mungu; nataka kushinda dhambi katika maisha yangu. Je! Lazima nifanye nini kwanza?

    Lazima ukumbuke vidokezo viwili vya muhimu sana. kwanza, moyo wa kiburi ungangana kupata wokovu; lakini cheo cha mbinguni na usawa wako wa kupatanishwa zinapatikana zote katika haki ya huyu mtu wa nje. Pili, Mungu hawezi kufanya cho chote kuwadia kupatanishwa kwako hadi, ukishasawishiwa unyonge wako, na kuvuliwa kujitegemea kibinafsi, ujitolee kwa utawala wa Mungu.

    Walakini, swali lako linamaanisha kuwa tayari umehukumika na dhambi zako za binafsi. Hauna furaha mwenyewe. Hatua ya kwanza ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wanamrudia Mungu ni kutubu. “Tubuni…mrejee, ili dhambi zenu zifutwe” Matendo 3:19. Tunahuzunika mara kwa mara kwasababu matendo yetu maovu yanatuletaa matokeo mabaya; lakini hii si toba. Toba ya kweli ni zaidi ya huzuni ya dhambi. Ni kubadilika kabisa kutoka kwa maovu. Hakuna toba ambayo ni ya kweli ambayo haifanyi ubadiliko. Haitoshi,je! Mwanadamu anaweza kutubu kivyake? Hawezi kujisamehe au kujikosoa. Toba ni sawa na zawadi ya Mungu kama vile msamaha, na haiwezi kupatikana isipokuwa kama ipewavyo moyo.

    Wakati moyo unatubu kabisa kwa kukubali ushawishi wa Roho wa Mungu, mwenye dhambi ataanza kufafanua utakatifu wa sheria takatifu ya Mungu. Kutakuwa na tamaa kuu ya kuishi maisha safi na matakatifu na kuwa kila wakati na amani na Mungu. Na tunapo ngangana kila siku kutembea karibu na Mungu, “Atasogea karibu”, na tabia zetu zitaonyesha Yeye zaidi na zaidi wakati njia zetu za zamani za dhambi “zikifa kila siku”. Yakobo 4:8; Wakorintho wa kwanza 15:31.

    Ushindi juu ya Dhambi kupitia Kristo

    21. Tafadhali fafanua zaidi juu ya kitambulisho cha mtu huyo wa nje; je! kwa kweli inawezekana kupitia yeye kupata ushindi juu ya dhambi tukiishi bado katika ulimwengu huu?

    Kulikuwa na mtu mmoja tu ambaye angeweza kukamilisha safari hii vikamilifu. Mtu huyo si mwingine mbali Mwana wa Mungu. Je! Ni kwanini Mwana wa Mungu ndiye mtu yule aliye hetimu safari hii peke yake? Kwasababu Mwana wa Muumbaji wa vitu vyote, “Ni mfano wa Mungu asiyeonekana…kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa.” Na Mwana anatabia na uweza wote wa Mungu kwasababu Yeye ni “chapa ya nafsi yake.” Kristo ana maisha ndani Yake, ambayo ni zaidi ya maisha yote ya wanadamu watakao zaliwa kwa pamoja na wakitaka kifo Chake cha mateso. Hivyo basi, kujitolea Kwake kungetimiza haki ya Mungu kwa wenye dhambi wote ambao wataitikia kifo chake cha mateso, akiwaonyesha huruma na upendo Wake. Katika Mwana, “Fadhili na kweli zimekutana; haki na amani zimebusiana.” Na akiwa sawa na Mungu, Mwana kwa kweli ndiye mtu peke yake ambaye angemfunulia mwanadamu mambo mazuri ya Mungu na kupatanisha mwanadamu na Mungu. Wakolosai 1:15, 16; Waebrania 1:3; Zaburi 85:10.

    Walakini, ili hii ifanyike, na ndiposa haki ya Mungu ikamilike, ilimbidi Mwana achukue umbo letu la uwanadamu lililo anguka kwa nafsi Yake, ambalo lilipendelea maovu. “Maana ni hakika, hatwai hasili ya malaika; ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.” Ni kwa hatua hiyo peke yake ndiyo ingekuwa sawa kwa Mwana kuwa kielelezo chetu chema. “akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake: Yeye hakutenda dhambi.” Waebrania 2:16 ; petro wa kwanza 2:21, 22.

    Kutoka kwa upande mmoja kupitia ukuu Wake anamguza Mungu na, kutoka kwa upande mwingine, kupitia ubinadamu Wake anamguza mwanadamu. hivyo basi,hakuna mwingine ila Mwana ambaye angeweza kupeana zawadi hii ya dhamana ya upatanisho. “Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu ya mwili, yeye [Mwana] naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo” “…Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake” “Kwa maana...tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake.” Kristo alichukua asili yetu ya kibinadamu kwa nafsi Yake ikiwa na udhahifu wote, na bado aliiishi maisha yasiyo kuwa na dhambi. Ni maisha ya ushindi juu ya dhambi ambayo Kristo anahamu ya kutupa nguvu tuweze tuishi. Waebrania 2:14; Wakorintho wa pili 5:19; Warumi 5:10 .

    Mapendekezo ya Mungu kwa watoto Wake ni ya juu zaidi ya pale mafikira ya juu sana ya mwanadamu yanaweza kufika. “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu” “...kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu,ninyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote” “Mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka…” “Tafuteni…utakatifu,ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”. Makubaliano Yake yote yanawezesha. Mungu hafanyi hitaji lo lote bila kufanya mpangilio wa kukamilika kwake. Mathayo 5:48; Petro wa kwanza 1:15;Wafilipi 2:15; Waebrania 12:14.

    “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. - Mathayo 5:48

    Hakuna ye yote apasaye kuanguka kufukia ukamilifu wa tabia ya Kikristo. Kwa kujitolea kwa Kristo, toleo lilifanywa la kila muumini kupokea zaidi na kwa wingi cho chote ambacho kinahitajikana ili kufikia lengo hili. Mungu anatuita sisi kufikia kiwango cha ukamilifu na sehemu, mbele yetu ni kielelezo cha tabia ya Kristo. Katika uwanadamu Wake, ukikamilishwa na maisha ya kukataa uwovu kila mara, Kristo alionyesha kuwa kupitia ushirikiano na Ukuu, wanadamu wanaweza katika maisha haya kufikia ukamilifu wa kitabia. Hii ni uhakikisho wa Mungu kwetu sisi pia, ili tupate ushindi.

    Tunamshukuru Mungu ambaye “atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo”Wakorintho wa kwanza 15:57.

    22. Kristo aliwezaje kuishi maisha yasiyo na dhambi katika ulimwengu huu wa maovu?

    Hakuna maisha mengine ambayo yalijawa na kazi na jukumu kama ya Kristo, Il hali alipatikana mara nyingi akiomba! Alizungumza na Mungu kila wakati! Tena na tena katika historia ya maisha Yake ulimwenguni rekodi zinapatikana kama hizi: “Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu. Akaomba huko” “Lakini yeye alikuwa akijiepa, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba” “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu” Marko 1:35; Luka 5:16; 6;12.

    Ushirikiano usiyo vunjika na Baba Yake ulikuwa wa maana sana kwa Kristo. Hivyo basi, inapaswa kuwa nasi wa leo. Kama mmoja nasi, mshiriki katika mahitaji yetu na udhahifu, alimtegemea Mungu vikamilifu, na katika sehemu ya siri ya maombi alitafuta nguvu kuu, ndiposa aweze kuenda akiwa tayari kwa kazi na majaribu. Katika ulimwengu wa dhambi Kristo alivumilia kungangana na mateso ya moyo. Katika ushirika na Mungu angeweza kutoa mzigo wa huzuni ambao ulikuwa ukimbonda. Hapa alipata pumziko na furaha. Kama mwanadamu aliabudu kiti cha enzi cha Mungu hadi uwanadamu Wake ukachajiwa na umeme wa mbinguni ambao iliunganisha uanadamu wake na ukuu. kupitia ushirika wa mara kwa mara alipokea nguvu za kuishi maisha yasiyo na dhambi. Masaibu Yake yanaweza kuwa yako.

    Kabla ya yote ni uwezekano wa ajabu wa kuwa kama Kristo, utiifu kwa kanuni zote za sheria ya Mungu. Lakini kivyetu sisi, hatuwezi. Utakatifu huu unapatikana peke yake kwa kujifundisha wenyewe kila wakati kujisalimisha kwa usawishi wa mafunzo ya Roho Mtakatifu. Nguvu ziwezavyo za Kristo zitatusaidia kuvumilia katika kushinda kila shida. Tunapaswa tumuombe Kristo bila kukoma, kama alivyokuwa akiwasilina na Baba Yake mara kwa mara, ili atusaidie kushinda udhahifu wetu wa kuridhi. Hali hii ya kutuosha kutokana na udhahifu ni ya kuendelea. Siku kwa siku, tunapaswa tushirikiane na Mungu, tukiweka mbele bidii yetu ya kuvumilia ili kupalilia tabia nzuri. Kristo atatupa kwa furaha nguvu tunazo hitaji na baraka katika mngangano wetu dhidi ya uwovu ambao utuvamia.

    Imani ndani ya Kristo pamoja na Bidii ya kibinafsi

    23. Je! Unasema kuwa imani ndani ya Kristo haiwezi kubadilisha bidii yangu ya kibinafsi ya kuanzisha vita bila kukoma dhidi ya dhambi? Je! Siwezi tu kuamini katika Kristo na kile alichonifanyia na hiyo itoshe kuokoka?

    Kila mmoja wetu anaye mpokea Kristo kama Mwokozi wake ana fursa ya kupokea tabia Zake. Walakini, wale ambao wanasubiri kupata mabadiliko ya haraka katika tabia zao bila bidii ya kuamua kushinda dhambi katika sehemu yao, watakasirika. Lazima tuwe waangalifu ili umbo letu la kitambo lisipokee ukuu tena, kwa kuwa shetani atabuni mitego ambapo tutakuwa tena mateka wake. Tunapaswa kutimiza “wokovu wetu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema”Wafilipi 2:12, 13.

    Kristo ametupa uhakikisho wa kuwa kufikia ukamilifu wa tabia ni rahisi. Tabia ya kupendeza, pande zote hairidhiwi. Haikuji kwetu kwa ajali. Tabia ya kupendeza inapatikana kwa bidii ya kibinafsi kupitia kustahili na nguvu za Kristo. Mungu upeana kipawa, nguvu za kiakili; sisi utengeneza tabia Utengenezwa kwa vita ngumu, kali ya kibinafsi. Mzozo baada ya mzozo lazima ianzishwe dhidi ya tabia za kuridhi.

    Itatubidi tujikemee wenyewe kwa karibu, na tusiruhusu tabia yo yote isiyo nzuri ibakie bila kurekebishwa. Wakati mwingine hii ni kazi inayo uma sana na huvunja moyo kwasababu, tunapo ona makosa katika tabi yetu, tunaendela kuangalia makosa hayo, wakati tunapaswa kumuangalia Yesu. Lakini, kila mmoja anaye ingia milango nyeupe ya mji wa Mungu ataingia hapo kama mshindi, na ushindi wake mkubwa utakuwa kujishinda mwenyewe.

    Mtu ye yote asiseme, siwezi rekebisha makosa katika tabia zangu. Kama ye yote atafikia uwamuzi huu, kwa kweli ataanguka katika kupata maisha ya milele. Ugumu upo katika mapenzi ya kibinafsi. Ugumu wa kweli utokea kwa ufisadi wa roho isiyo takaswa, na kutokutaka kujisalimisha kwa utawala wa Mungu.

    Kutii Bwana ni ya maana sana unapo tembea na Yeye. Tabia mbili za maana sana za muumini ni kutii sheria Yake, na imani ya Kristo Angalia Ufunuo 14:12. Kwa hivyo “kuamini” Kristo tu haitoshi. Ingekuwa hivyo, basi Shetani mwenyewe angepata mbingu, kwasababu imeandikwa, “mashetani nao waamini na kutetemeka”Yakobo 2:19

    kwa mfano, ni nini iliwasababisha Adamu na Hawa kutolewa Edeni? Hawakuwa na shida ya kumuamini Yesu kwa kuwa alitembea nao mchana. Angalia Mwanzo 3:8. Ni kuto kutii ambako kuliwaharibia kabisa. Hivyo basi, tunaokolewa kwa matendo? “Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali kwa rehema yake alituokoa” Tito 3:5. Hatutunzi sheria ili tuokolewe. Kutunza amri ni matunda ambayo Kristo alisema wafuasi wake wataonyesha.

    Sheria inadhibitisha kuwa tunahitaji Mwokozi. Tukiangalia sheria kama “kioo” cha Wakristo, tunaweza kuona kasoro yetu vizuri zaidi. Angalia Yakobo 1:23-25. Inatufanya tutambue kuwa hatuwezi kupata ukamilifu bila Kristo. Sheria haiwezi kuokoa. Inaweza kudokeza tu hitaji letu la Mwokozi. Ili kuonyeshana, Kama ungeanguka katika kiziwa cha matope, ukisimama mbele ya kioo utaona uchafu wako. Je! Kioo kinaweza kukuosha? Hapana, hakiwezi. Kinaweza kudoze tu hitaji lako ya kuoshwa.

    24 . Je! inawezekana kweli kuwa nikiamini nguvu za Kristo pamoja na vita visivyo isha vya kibinafsi dhidi ya kasoro zangu zote za kibinafsi, tabia yangu itakamilika?

    Malaika wa mbinguni watafanya kazi na ye yote anayetafuta tabia yake kukamilika. Kwa kila mmoja anaye husika katika kazi hii Kristo anasema, Niko mkononi mwako wa kuume ili kukusaidia “maana pasipo mimi [Yesu] ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”Yohana 15:5. Kumbuka hii. Wacha tuwe watu wa kweli kama vile sindano kwenye ufito ili majaribu yo yote isituharibu. Wacha tusimkasirishe Yeye ambaye alitupenda sana mbaka akapeana maisha yake mwenyewe ili kutulipia dhambi zetu.

    Kama umefanya makosa, kwa kweli utapata ushindi ukiweza kuona makosa haya na kuyachukilia kama ishara ya onyo. Hivyo basi,unabadilisha kushindwa kuwa ushindi, kumkasirisha adui na kumsujudia Mwokozi wako.Baadaye,wakati mapenzi yako yakishirikina na mapenzi ya Mungu, inakuwa yenye nguvu.

    Mtengenezaji wa mahali Palipobomoka

    25. Sasa ninakubali umaana wa kuelewa ni nani ambaye ni mnyama, chapa yake, na sanamu yake, kwasababu ukamilifu ungekuwa mgumu kama ningedanganywa nikeuke sheria ya Mungu. Je! Ninaweza kufanya nini sasa?

    Sasa tumekuja kujua kuwa Jumapili ni chapa ya papa (mnyama), na kuwa Shetani hivi karibuni hataifanya kuwa vigumu kwa watu kusujudu siku ya kupumzika ya saba ya Mungu ambayo ni takatifu kwa kutumia Marekani kupitisha sheria ya Jumapili duniani kote. Tunapaswa kuanza kusujudu Sabato (kujivunza wenyewe wakati nyakati ni rahisi) na kushiriki ukweli huu na wengine ili tujaribu kupata mioyo nyingi kama tuwezavyo.

    Amri imepeanwa, “Piga kelele, usiache, paza sauti yako kama tarumbeta, uwahubiri watu wangu kosa lao…” Si dunia ya wapagani, mbali wale ambao Bwana aliwateuwa kama “watu wangu,” ambao watakemewa kwa makosa yao. Anasema zaidi, “Walakini wanitafuta kila siku, hupenda kujua njia zangu, kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki, hufurahi kumkaribia Mungu”Isaya 58:1,2.

    Hapa kuna watu ambao wanajidhania kuwa wenye haki, na uonyesha kuwa na hamu katika huduma ya Mungu; lakini kemeo kali la Mungu uwakosoa kwa kukanyagia juu ya mafunzo makuu.

    Nabii Isaya, anadokeza sheria gani ambayo imesaulika: “…nawe utaitwa, mwenye kutengeneneza mahali palipobomoka… kama ukigeuza mguu wako usiihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu, ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima, ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe: Ndipo utakapojifurahisha katika Bwana”Isaya 58:12-14.

    Hivi karibuni, kupitia sheria za Jumapili duniani, Shetani ataifanya kuwa makosa kumtii Mungu

    Hii pia inatumika kwako. Kubomoka huku kulifanywa kwenye sheria ya Mungu wakati Sabato ilibadilishwa na Kanisa la Kikatoliki la Kirumi. Wakati umefika wa shirika kuu kurejeshwa. Mahali palipobomoka panaswa kutengenezwa. Tumeamua kuwa kati ya wale ambao watatengekeza mahali palipobomoka. Je! Ungetaka kuwa mtengenezaji wa mahali palipobomoka?

    Je! Ungetaka kuanza kuweka Jumamosi takatifu, kwa kuepuka kutofanya kazi yako, usitafute raha yako,na usizungumze maneno yako mwenyewe wakati wa masaa takatifu ya siku ya Bwana ya Sabato?

    Mahali pa kuabudu

    26. Ndiyo,ningeheshimika sana kuwa mtengenezaji wa mahali palipobomika katika sheria ya Mungu. Walakini, sijui kanisa lo lote ambalo linasujudu kwa kweli Sabato, linalo fuata Biblia peke yake, na kumfunua papa. Hivyo basi nitaabudu wapi?

    Kuwa na uhakika kuwa haukabili kuchanganyikiwa huku peke yako. Wale wanao husika na mradi huu, wamekabiliana na hali hii. Ilitubidi tuwache makanisa yetu wakati tulipogundua vile wanavyopenda ukweli kwa uchache. Hata makanisa yanayo dai kusujudu Sabato wanapayuka tu. Wanaweka Sabato takatifu wakati inawezekana au inastahili kufanya hivyo. Wakati hali zinazozuiya zitokeapo, zinazofanya kuzingatia Sabato kuwa vigumu, makanisa haya huwafukuza washirika wake kutoka kwa kazi yao ili kuweka Sabato takatifu. Lakini Neno la Mungu linatuambia, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”Matendo 5:29

    Hivi karibuni, kupitia sheria za Jumapili duniani, Shetani ataifanya kuwa makosa kumtii Mungu. Lazima tuwe tayari kuhesabiwa kama waalifu kwa kuweka siku ya Sabato takatifu, Badala ya kufuata sheria ya mwanadamu na kuwa na hatia ya kutomtii Mungu. Hivi karibuni kila mtu ulimwenguni atakabiliwa na kuchanganikiwa huku. Je! Nitamtii nani, mwanadamu au Mungu? Tumechagua kumtii Mungu haijalishi usawishi na gadhabu tutakayopewa kwa kuwa tunatafuta ufalme wa mbinguni.

    Kwa sasa, baada ya kuwacha makanisa yote na kidini inayopinga ukweli wa Mungu, tukaanza kuabudu manyumbani kwetu tukijaribu kupata jamii, marafiki, na majirani kwa ukweli hadi tukaanzisha ushirika mdogo wa waumini. Hivyo basi, tunaweza kudai kuwa Kristo ahidi “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yako”Mathayo 18:20.

    Tunashuhudia kuwa wakati tumejitenga na makinisa na dini za uongo katika kutii amri ya Mungu (angalia swali la 18) tunafurahiya uhuru na kufunguliwa. “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” Yohana 8:32. Wacha furaha yetu iwe yenu, unapoamua kujitenga ili kuwa mwana wa kiume au wa kike wa Mungu. “Yeye ashindaye atayarithi haya”Ufunuo 21:7.

    -----------------------

    Tunaomba kuwa utachagua kuwa mtengenezaji wa mahali palipobomoka katika sheria ya Mungu, na utashughulika kuwaokoa wengi wanaotaka kutokana na kupotoka kunao vamia ulimwengu unao kabili nafasi yake ya mwisho kabla ya kuja kwa pili hivi karibuni kwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. AMINA.

    Mistari yote ya Biblia imetolewa kutoka kwa Tafsri ya Kiugunja.

    Mistari yote ya Biblia imetolewa kutoka kwa Tafsri ya Mfalme Yakobo. Ili kutumiwa nakala ya jalada ya “Vita Vikuu” (kitabu kinacho fafanua zaidi kwa ukamilifu yaliyoshirikiwa katika nakala hii), au kupata nakala ya jalada ya “Hamu ya Maisha” (kitabu kuhusu maisha ya Yesu) tafadhali wasiliani nasi kwa www.worldslastchance.com